Uchumi wa Marekani bado hauridhishi

Imebadilishwa: 31 Agosti, 2012 - Saa 16:20 GMT

Mwenyekiti wa benki kuu nchini Marekani Ben Bernanke, ametaja hali ya uchumi wa Marekani kama ya kutoridhisha

Bwana Bernanke aliambia mkutano wa maafisa wa benki kuu pamoja na wanazuoni kuwa benki kuu ya Marekani itachukua hatua za ziada kuimarisha uchumi ingawa hakutaja hatua zitakazochukuliwa.

Hotuba ya Bernanke imetizamwa kwa karibu kuona hatua ambazo benki hiyo itaweza kuchukua kuuchepua uchumi zaidi.

Baadhi ya mambo yanayoweza kufanyika ni kuongeza uchapishaji wa sarafu na kununua hawala za serikali hatua inayoweza kuuchepua uchumi kwa muda.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.