Uingereza imekosa kupiga tanji mali

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 10:24 GMT

BBC imegundua kuwa serikali ya Uingereza imekosa kupiga tanji mali za washirika wa karibu wa uliokuwa utawala wa Misri chini ya aliyekuwa rais Hosni Mubarak.

Uchunguzi uliofanywa na idhaa ya kiarabu ya shirika hilo, ulionyesha kuwa mali pamoja na biashara kubwa kubwa zinazomilikiwa na washirika wa rais wa zamani, hazijaathirika hata kidogo na vikwazo.

Rekodi zinaonyesha kuwa mwanawe Mubarak angali anamiliki nyumba yake ya kifahari iliyoko mjini London.

Mke wa waziri mmoja wa zamani pia aliweza kusajili kampuni moja mjini London mwezi Novemba mwaka jana.

Ikijibu tuhuma hizo, serikali ya Uingereza, imesema kuwa mali za washirika hao haiwezi kupigwa tanji ikiwa bado washirika hao hawajahusishwa na uhalifu wowote na ikiwa pia amri ya kupiga tanji mali hizo kisheria bado haijatolewa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.