Makampuni ya mbao yahujumu sheria Liberia

Imebadilishwa: 4 Septemba, 2012 - Saa 08:18 GMT


Shirika la Global Witness, linasema kuwa robo ya ardhi nchini Liberia imetolewa kwa makampuni ya kukata mbao katika kipindi cha miaka miwili kufuatia kile inachosema ni kutolewa kwa siri vibali haramu vya kukata mbao.

Mikataba hiyo mipya inayojulikana kama vibali vya matumizi binafsi, kimsingi vilitolewa ili kuwaruhusu wamiliki binafsi wa ardhi kukata miti katika mashamba yao.

Hatua ambayo shirika la Global Witness linasema makampuni yanahujumu sheria kwa kutumia vibali haramu vya kukata miti huku yakikwepa sheria za utenda kazi na kuzuia manufaa kwa jamii zinazoishi katika maeneo hayo.

Rais Ellen Johnson Sirleaf, ameamuru uchunguzi kufanya kuhusiana na kashfa hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.