Mabadiliko ya mawaziri Uingereza

Imebadilishwa: 4 Septemba, 2012 - Saa 12:35 GMT

Waziri mkuu wa uingereza David Cameron amefanya mabadiliko ya kwanza makubwa katika baraza lake la mawaziri tangu alipoingia mamlakani.

Kama ilivyotarajiwa alipuuza wito wa kutaka amuachishe kazi waziri wa fedha George Osborne kutokana na kudumaa kwa uchumi.

Waziri Jeremy Hunt ambaye alifanikisha mashindano ya olimpiki amepandishwa cheo na kuwa waziri wa afya licha ya madai kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na himaya ya habari ya Rupert Murdoch wakati akiwa waziri wa utamaduni.

Katika mabadiliko mengine mwanasiasa mzoefu Kenneth Clarke amepoteza wadhifa wake wa waziri wa sheria ingawa atasalia katika baraza la mawaziri.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.