Shinikizo mpya dhidi ya rais Assad

Imebadilishwa: 5 Septemba, 2012 - Saa 11:09 GMT

Rais wa Syria Bashar al-Assad, anakabiliwa na shinikizo mpya kutoka kwa jamii ya kimataifa aachie madaraka, huku serikali za ukanda huo zikiikashifu serikali yake.

Rais wa Misri, Mohammed Morsi, aliambia mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya nchi za kiarabau kwamba muda umewadia wa mageuzi nchini Syria.

Rais alisema kuwa Assad anapaswa kujifunza kutokana na matukio ya mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika katika ukanda huo katika miezi ya karibuni.

Waziri mkuu wa uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa Syria sasa imekuwa serikali ya kigaidi.

Siku ya Jumanne mjumbe maalum kuhusu Syria, Lakhdar Brahimi,alisema kuwa idadi ya watu ambao wameuawa katika mgogoro huo wa kisiasa ni kubwa sana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.