Mfalme amuombea mkewe kasri

Imebadilishwa: 6 Septemba, 2012 - Saa 12:46 GMT

Mfalme wa Zulu

Mfalme wa kabila la Zulu nchini Afrika Kusini Goodwill Zwelithini, anaitaka serikali kutumia dola laki saba kumjengea mkewe wa sita kasri lake binafsi,.

Malkia Zola Mafu, ambaye ni mkewe wa mwisho anaishi na mmoja wa wake za mfalme huyo.

Serikali ya jimbo la KwaZulu Natal mojawapo ya majimbo tisa tayari imefanya makadirio ya bajeti ya familia ya kifalme mwaka huu.

Vyama vya upinzani, vimekuwa vikimtuhumu mfalme huyo pamoja na wake zake na watoto wao zaidi ya 25, kwa kufuja mali ya umma.

Mfalme Zwelithini, ambaye ni kiongozi wa kabila kubwa zaidi Afrika Kusini, ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa nchini humo.

Idara ya wizara ya fedha kuhusiana na familia ya kifalme, Mduduzi Mthembu, aliambia kamati ya bunge kuwa takriban dola 700,000 zinahitajika kumjengea malkia Mafu kasri lake.

Idara hiyo pia inataka,pesa za ziada dola milioni 1.4 kulikarabati kasri la mke mwingine wa mfalme huyo MaMchiza.

Inaarifiwa kuwa gharama ya shughuli hizo itatolewa katika kipindi cha miaka mitatu.

Wabunge wa kamati hio walisema kuwa watatathmini ombi hilo baadaye mwezi huu.

Malkia Mafu aligonga vichwa vya habari alipoonekana na mfalme Zwelithini mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka kumi na minne.

Mwaka 2008, vyama vya upinzani vilikosoa wake za mfalme huyo kwa kutumia dola 24,000 kununua nguo za kitani na kwenda likizo za bei ghali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.