Wanajeshi 25 wafariki nchini Uturuki

Imebadilishwa: 6 Septemba, 2012 - Saa 09:09 GMT

Wanajeshi ishirini na watano wamefariki katika mlipuko uliotokea kwenye ghala la silaha.

Wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.

Mlipuko huo ulitokea wakati wanajeshi hao wakisongesha maguruneti.

Haijulikani kilichosababisha mlipuko wenyewe katika mkoa wa Magharibi wa Afyon, ingawa maafisa wanasema kuna uwezekano ilikuwa ni ajali tu.

Maafisa wa jeshi wamesema kuwa maguruneti yalikuwa yametapakaa kote katika eneo la tukio kutokana na nguvu za mlipuko huo na kuwaonya watu dhidi ya kwenda katika eneo hilo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.