Pakistan yafukuza shirika la misaada

Imebadilishwa: 6 Septemba, 2012 - Saa 08:55 GMT

Shirika la kimataifa la Save the Children, linasema kuwa serikali ya Pakistan imewataka wafanyakazi wake kuondoka nchini humo katika muda wa wiki mbili zijazo.

Hata hivyo linasema Pakistan haijatoa sababu ya uamuzi wake.

Maafisa wa Pakistan wamekuwa wakituhumu shirika hilo kwa kutumiwa kwa upelelezi na shirika la ujasusi la Marekani CIA katika kumsaka Osama bin Laden, madai ambayo shirika hilo limekuwa likikana .

Save the Children linasema kuwa lina takriban wafanyakazi elfu mbili nchini Pakistan na kwamba ni sita peke yao ambao ni wafanyakazi wa kigeni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.