Jasusi wa mauaji ya kidini auawa Pakistan

Imebadilishwa: 7 Septemba, 2012 - Saa 15:01 GMT

Afisa mwandamizi wa polisi nchini Pakistan, ambaye alikuwa akipeleleza mfululizo wa mauaji yanayohusiana na masuala ya kidini katika jimbo la Baluchistan, ameuawa kwa kupigwa risasi.

Jamil Kakar alikuwa akisafiri kwa gari katika mji mkuu wa jimbo hilo, Quetta, wakati watu waliokuwa katika pikipiki walipomfyatulia risasi.

Alikuwa akifuatilia kesi kadha ambapo waumini kadha wa madhehebu ya Shia waliuawa, na wapiganaji wa madhehebu ya Sunni.

Inasemekana kuwa zaidi ya Washia mia tatu nchini Pakistan wameuawa mwaka huu katika mashambulio yanayowalenga.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.