Waandishi habari wabughudhiwa Madagascar

Imebadilishwa: 8 Septemba, 2012 - Saa 14:46 GMT

Jumuia ya waandishi wa habari wa Madagascar inasema kuwa wanachama wake wanazidi kubughudhiwa na wakuu wa serikali na baadhi ya wananchi pia.


Jumuia hiyo, Association des Journalistes de la Presse Privee de Madagascar, imesema inawaunga mkono waandishi wa habari watatu ambao wamepewa hifadhi kwenye ubalozi wa Afrika Kusini nchini Madagascar.


Ubalozi ulithibitisha siku ya Ijumaa kuwa, watu hao watatu, ambao walikuwa wakifanya kazi katika kituo cha redio cha upinzani ambacho sasa kimefungwa, walipewa hifadhi mwezi uliopita.
Jumuia imesema waandishi hao wa habari wamekuwa wakibughudhiwa kwa muda mrefu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.