Watu 16 wauawa Afghanistan

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 14:42 GMT

Takriban watu 16 wakiwemo maafisa 11 wa polisi wameuawa kwenye shambulio la bomu la kujilipua Kaskazini Mashariki mwa Afghanistan.

Shambulio hilo lilitokea katika eneo moja lenye idadi kubwa ya raia katika mji wa Kunduz.

Idara ya polisi nchini humo imesema, takriban watu ishirini wengi wao raia walijeruhiwa.

Naibu kamanda wa polisi katika mji huo ameiambia BBC, kuwa mshambuliaji huyo aliwalenga maafisa wa polisi ambao walikuwa wamekusanyika kushika doria wakati wa maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika katika eneo hilo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.