Akamatwa kwa kuikejeli bendera India.

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 13:30 GMT

Mahakama moja mjini Mumbai, India, imeamuru mchora vibonzo anayekabiliwa na kosa la uchochezi pamoja na kuihujumu bendera ya nchi akamatwe na kuzuiliwa kwa wiki mbili.

Kukamatwa kwa Aseem Trivedi, kulizua hasira ya umma.

Moja ya michoro yake ya vibonzo amewachora mbwa mwitu watatu kwa bendera ya nchi badala ya simba watatu ambayo ndio nembo rasmi ya bendera ya nchi

Bwana Trivedi anasema kuwa michoro yake inanuia kutahadharisha umma kuhusu ufisadi serikalini.

Wakereketwa wa haki za binadamu pamoja na mkuu wa baraza la habari nchini humo ni miongoni mwa wale waliokemea hatua ya kukamatwa kwake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.