Uturuki haitamkabidhi Tariq al-Hashemi Iraq

Imebadilishwa: 11 Septemba, 2012 - Saa 08:55 GMT

Uturuki imesema haitamtoa makamu wa rais wa iraq Tariq al-Hashemi ambaye amekimbilia nchi hiyo.

Bwana Al-Hashemi ilihukumiwa kifo bila kuwepo hiyo siku ya jumapili kwa kufadhili makundi ya kigaidi.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliwaambia wanahabari kuwa bwana Al-Hashemi yuko huru kusalia nchini humo kama atakavyo.

Bwana al-Hashemi mwislamu wa madhehebu ya sunni alitorokea nchini Iraq mapema mwaka huu.

Alipuuzilia mbali kesi dhidi yake akisema imechochewa kisiasa na kusema kuwa aterejea nchini iraq iwapo tu kutakuwa na kile alichokitaja kama mahakama huru na ya haki.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.