Jeshi latahadharishwa Afrika Kusini

Imebadilishwa: 12 Septemba, 2012 - Saa 10:19 GMT

Jeshi la Afrika Kusini limewekwa katika hali ya tahadhari kubwa kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Hatua hii ni kwa maandalizi ya hotuba ya aliyekuwa kiongozi wa vijana katika chama tawala ANC Julius Malema.

Waziri wa Ulinzi , Nosiviwe Mapisa-Nqakula, amemuonya kiongozi huyo aliyefukuzwa kutoka ANC, dhidi ya kuzua vurugu lolote hatua ambayo amesema huenda ikawa na athari mbaya.

Bwana Malema anaripotiwa kujiandaa kuhutubia wanajeshi wanaokabiliwa na makosa ya ukosefu wa nidhamu yanayohusishwa na maandamano yaliyofanywa mwaka 2009 kuhusiana na mishahara na mazingira ya kazi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.