Rais Obama alaani mashambulizi Libya

Imebadilishwa: 12 Septemba, 2012 - Saa 13:56 GMT

Rais wa Marekani Barack Obama amelaani vikali shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi Libya hapo jana.

Katika taarifa ya Obama iliyothibitisha kuuawa kwa balozi huyo, Christopher Stevens, pia ilisema wamerekani wengine watatu waliuawa wakati wa shambulio hilo.

Ubalozi uliteketezwa na watu waliokuwa wamejihami kwa makombora na maguruneti wakati wa maandamano ya kulaani filamu ya Marekani ambayo walisema ilimkejeli Mtume Muhammed.

Spika wa bunge Mohammed Magarief, ameomba radhi kwa Marekani kufuatia mashambulizi hayo na mauaji yaliyofuata.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.