Vita dhidi ya mihadarati Mexico

Imebadilishwa: 13 Septemba, 2012 - Saa 09:47 GMT

Jeshi la wanamaji la Mexico linasema kuwa majeshi yake yamemkamata mtu anayeaminika kuwa kiongozi wa genge moja mashuhuri la kuuza madawa ya kulevya kaskazini mwa jimbo la Tamaulipas,mpakani mwa Marekani na nchi hiyo.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, Jorge Costilla, anayejulikana kwa jina lengine kama "El Coss," alikamatwa na kuzuiliwa mjini Tampico Kaskazini Mashariki mwa Mexico.

Costilla aliongoza vita vya udhibiti wa biashara za mihadarati katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Mexico kutoka kwa genge hasimu la Los Zetas.

Mapema Jumatano, polisi nchini Mexico walitangza kumkamata kiongozi mwingine wa biashara hiyo na ambaye anadaiwa kuwa mwasisi wa genge la majambazi la "The Resistance".

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.