Ombi la Obama kwa Misri na Libya

Imebadilishwa: 13 Septemba, 2012 - Saa 10:04 GMT

Rais wa Misri Mohammed Morsi, amesema kuwa hasira na ghadhabu zimetanda katika nchi za kiarabu dhidi ya filamu ya Marekani ambayo imetusi dini ya kiisilamu.

Lakini ameahidi kuwalinda wageni pamoja na balozi za Marekani dhidi ya mashambulizi.

Rais Obama alimpigia simu rais Morsi pamoja na mwezake wa Libya na kuwataka kushirikiana na Marekani kuwalinda wafanyakazi wake wa kigeni.

Ombi hili linafuatia shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi na kusababisha kifo cha balozi Christopher Stevens pamoja na maafisa wengine wanne wa ubalozi.

Maafisa wa Marekani wametaja shambulizi hilo kama tete na ambalo lilipangwa. Kuna tetesi kuwa huenda ni makundi ya jihad yalihusika na mashambulizi hayo

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.