Japan kusitisha matumizi ya Nuklya

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 11:05 GMT

Japan imezindua mpango wa kusitisha matumizi ya kawi ya nuklya katika kipindi cha miaka thelathini ijayo.

Ni katika mageuzi makubwa zaidi ya sera ya umma baada ya mkasa wa Nuklya katika kinu cha Fukushima mwaka uliopita kufanywa nchini Japan.

Katika mapendekezo yaliyotolewa na jopo la serikali, vinu ambavyo vilikuwa vikizalisha thuluthi moja ya kawi nchini Japan vitafungwa kabisa ifikapo mwaka 2040.

Miezi kumi na minane iliyopita, kinu cha nukyla cha Fukushima, Daiichi, kiliharibiwa na tetemeko la ardhi pamoja na Tsunami na kuzua mkasa mkubwa wa kinuklya baada ya miaka mingi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.