Mgomo wa walimu Chicago kuendelea

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 07:32 GMT

Vyama vya walimu mjini Chicago nchini Marekani, vimeamua kuendelea na mgomo wao wa wiki moja kwa siku zingine mbili wakati viongozi wao wakishauriana na wanachama takriban elfu ishirini na moja kuhusu mkataba walioafikia na meya wa mji huo Rahm Emanuel.

Mgomo huo wa walimu ni aibu kubwa kwa rais Barack Obama,hasa kwa sababu unafanyika katika jimbo lake na pia ikizingatiwa kuwa ni wakati wa kampeini za uchaguzi wa urais ambao na yeye anagombea muhula wa pili.

Meya wa mji huo, amekuwa akijaribu kufunga shule za kibinafsi na mahala pake kuweka shule za umma ambazo serikali inalipia na ambazo hazitazingatia sheria na kanuni nyingi, hatua ambayo inapingwa na walimu hao.

Meya huyo amesema kuwa sasa atataka ushauri wa mahakama ili kuharamisha mgomo huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.