Maandamano zaidi China dhidi ya Japan

Imebadilishwa: 18 Septemba, 2012 - Saa 10:28 GMT

Maandamano ya kuipinga Japan yameendelea kote nchini Uchina , huku makampuni mengi ya Kijapani yaliyoko uchina yakifungwa kwa muda baada ya siku kadhaa za ghasia.

Maelfu ya watu wameandamana huku wakipita kwenye ubalozi wa Japan mjini Beijing , wakionyesha hasira yao juu ya mpaka unaozozaniwa baina ya nchi hizo kwenye bahari ya Mashariki mwa uchina

China pia inaadhimisha vita vyake vya kurejesha mikononi mwa Uchina eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo lililovamiwa na Japan miaka ya thelathini..

Uchina ilipinga kutua kwa muda kwa raia wa Japan katika kisiwa kinachozozaniwa na nchi mbili kijulikanacho kama Senkaku nchini Japan na Diaoyu kilichoko Uchina.

Walinzi wa mwambao wa Japan wako katika hali ya tahadhari kufuatia idadi kubwa ya mashua za uvuvi za kichina zinazoripotiwa kuelekea huko.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.