NATO kupunguza harakati zake

Imebadilishwa: 18 Septemba, 2012 - Saa 10:19 GMT

Vikosi vya vya nchi za Magharibi vya kujihami NATO nchini Afghanistan, vinasema vinapunguza kwa kiwango kikubwa harakati za pamoja na jeshi la Afghanistan kutokana na kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha mashambulio dhidi ya wanajeshi wa NATO yanayofanywa na wanajeshi wa Afghanistan.

Msemaji mmoja wa NATO ameeleza kwamba katika siku zijazo, ushirikiano wa aina hiyo utafanyika katika kiwango cha kikosi cha batalion, ambayo ni operesheni kubwa inayohusisha mamia ya wanajeshi.

Harakati nyingine ndogo za kijeshi bado huenda zikafanyika, lakini itabidi zikaguliwe na makamanda wakuu.

Tayari zaidi ya wanajeshi 50 wa NATO wameuawa na wanajeshi na Polisi ya Afghanistan mwaka huu, 15 kati yao ikiwa ni katika mwezi Agosti pekee.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.