Taasisi mpya huru kuhusu nyuklia Japan

Imebadilishwa: 19 Septemba, 2012 - Saa 08:15 GMT

Japan imezindua taasisi mpya huru ya ukaguzi wa nuklia kufuatia mkasa katika kinu cha nuklia cha Fukushima uliosababishwa na tsunami kubwa mwaka jana.

Taasisi hiyo mpya imeteuliwa kufuatia kuwepo kwa shutuma kwamba mgongano kati ya wakaguzi wa nuklia na waendeshaji vinu hivyo, ulichangia kuyeyuka na kumwagika kwa nuklia katika kinu cha Fukushima.

Hata hivyo wataalamu wanasema taasisi hiyo inakosa mamlaka halisi, na mkuu wake mpya ni mtu anayehusika na viwanda vya nuklia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.