Rais Obama amkashifu Romney kwa ubaguzi

Imebadilishwa: 19 Septemba, 2012 - Saa 07:50 GMT

Rais wa Marekani Barack Obama amemshtumu mpinzani wake wa chama cha Republican, katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba Mitt Romney, kwa kubagua sehemu kubwa ya raia wa Marekani.

Bwana Romney alinaswa kisiri kwenye ukanda wa video akitoa matamshi ya kuwadharau baaadhi ya wapiga kura wakati wa hafla ya faragha ya kuchangisha pesa za kampeni katika chama cha Republican.

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi kimoja cha televisheni nchini Marekani Obama amesema jambo ambalo amejifunza akiwa rais ni kuwatumikia wamarekani wote.

Baada ya kuchaguliwa , alisema , atajitahidi kuwahudumia hata wale ambao hawakumpigia kura.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.