Maandamano makubwa nchini India

Imebadilishwa: 20 Septemba, 2012 - Saa 12:41 GMT

Serikali ya India inakabiliwa na mzozo wa kisiasa baada ya kuidhinisha mageuzi makubwa ya kiuchumi wiki iliyopita.

Vyama vya upinzani na vyama vya wafanyakazi vinaandamana hii leo kupinga kupandishwa kwa kiwango kikubwa cha bei ya mafuta na ufunguzi wa sekta ya biashara kwa masoko ya kigeni kama vile Wal- Mart na Tesco.

Waandalizi walisema wanatarajia mamilioni ya watu kushiriki katika maandamano hayo.

Wafanyakazi walizuia njia za reli katika majimbo ya Uttar Pradesh na Bihar huku shughuli zikisitishwa katika ngome za upinzani katika majimbo ya Calcutta na Bangalore .

Lakini waandamanaji hawakujitokeza kwa wingi katika miji ya Delhi na Mumbai.

Chama cha Congress kinaamini kuwa maandamano hayo ni shinikizo muhimu kwa mageuzi nchini humo ingawa wadadisi wanasema kuwa mageuzi hayo yatatishia maisha ya kawaida ya mamilioni ya watu katika sekta hiyo ambayo haina mpangilio.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.