Jeshi ladhibiti maandamano Pakistan

Imebadilishwa: 20 Septemba, 2012 - Saa 14:36 GMT

Utawala nchini Pakistan umelazimika kuwaita wanajeshi kuthibiti maelfu ya watu wanaoandamana katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad kupinga filamu iliyotengenezwa nchini Marekani, inayomkejeli Mtume Muhammad .

Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi kuwatawanya waandamanaji hao, wengi wao wakiwa ni wanafunzi waliokuwa wakijaribu kufika katika eneo lenye ulinzi mkali ambalo ofisi nyingi za kibalozi zipo.

Picha za televisheni zimeonyesha waandamanaji hao wakipambana na maafisa wa polisi.
Ripoti zinasema watu kadhaa wamejeruhiwa kwenye machafuko hayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.