Kifo cha daktari wa Nazi kuchunguzwa

Imebadilishwa: 21 Septemba, 2012 - Saa 14:15 GMT

Mahakama moja nchini Ujerumani imeakhirisha kwa muda uchunguzi kuhusu mauaji ya mshukiwa wa Nazi Aribert Heim, anayetakikana sana kwa uhalifu wa kivita.

Inaaminika Heim aliwaua mamia ya wafungwa waliokuwa wanazuiliwa katika kambi za mateso

Mahakama ilisema kuwa hakuna shaka kwamba Heim, raia wa Austria aliuawa nchini Misri miaka ishirini iliyopita.

Heim alijulikana kama daktari wa kifo na inaarifiwa aliwatumia wafungwa wa kiyahudi waliokuwa katika kambi ya Mauthauen kwa majiribio ya kimatibabu wakati wa vita vya pili vya dunia.

Aidha alifanya kazi yake nchini Ujerumani hadi mwaka 1962, wakati ambapo aliripotiwa kutoroka pindi alipopata habari kuwa alikuwa anasakwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.