Mkutano wa mzozo kati ya China na Japan

Imebadilishwa: 25 Septemba, 2012 - Saa 09:48 GMT

Uchina na Japan zinafanya mazungumzo ya hali ya juu kuhusiana na visiwa vinavyozozaniwa katika ziwa la China Mashariki.

Mkutano huu ni wa kwanza tangu kuanza kwa mzozo huu nchini China mapema mwezi huu.

Kulingana na taarifa kwenye mtandao wa wizara ya mambo ya nje wa China, naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Zhang Zhijun, amemuonya mwenzake wa Japan kuwa China haitaruhusu ukiukwaji wowote wa uhuru wa eneo lake.

Mkutano huo unaoendelea mjini Beijing, unakuja wakati takriban mitumbwi sitini kutoka Taiwan ikisindikizwa na manowari za kijeshi kuingia katika visiwa hivyo vinavyozozaniwa upande wa China.

Msafara huo wenye wavuvi karibu mia tatu uko katika maeneo ambayo Japan inamesema yanafaa kuwa na ulinzi.

Mitumbwi hiyo iko na wanamaji wa Taiwan.

Kisiwa hicho chenye utata --kinachoitwa Senkaku nchini Japan na Dia oyutai nchini Uchina -- kinadaiwa na Uchina, Japan na Taiwan.

Uhusiano kati ya Uchina na Japan umeharibika katika wiki za hivi karibuni baada ya serikali ya Japan kununua visiwa vitatu kutoka kwa mmiliki binafsi.

Uhasama wa hivi karibuni umetokea wakati wanadiplomasia wakuu kutoka nchi zote mbili wanakutana mjini Beijing kujadili mzozo wa mpaka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.