Mageuzi ya sheria yakataliwa Kuwait

Imebadilishwa: 25 Septemba, 2012 - Saa 10:52 GMT

Mahakama ya kikatiba nchini Kuwait imekataa hoja ya serikali kuhusu sheria ya uchaguzi nchini humo katika kile kinachoonekana kama ushindi kwa chama cha upinzani chenye kufuata misingi ya kiisilamu.

Serikali ilitaka kuifanyia mageuzi sheria ya uchaguzi hasa ikilenga majimbo ya nchi katika hatua ambayo upinzani ulisema inapendelea wagombea wa serikali.

Viongozi wa nchi hiyo ambao wanaungwa mkono na nchi za Magharibi, walifunga vikao vya bunge baada ya chama cha upinzani kushinda viti vingi vya bunge katika uchaguzi uliofanyika mwezi Februari.

Haijulikani ni lini uchaguzi utakafanyika.

Kuwait ndio nchi yenye bunge lenye hamasa kubwa za kisiasa ikilinganishwa na mabunge mengine katika ghuba ya uwajemi ambalo hutofautiana wazi na sera za serikali pamoja na kupinga ufisadi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.