Matamshi ya waziri yamletea msamaha

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 15:04 GMT

Wapiganaji wa Taleban nchini Pakistan, wanasema wamemsamehe waziri mmoja wa serikali ambaye aliahidi zawadi ya pesa kwa yeyote atakaye muua mtu aliyetengeza filamu ya kuidhihaki dini ya kiisilamu.

Filamu hiyo iliyotengezwa nchini Marekani ilisababisha hasira miongoni mwa waisilamu ambao walizua vurugu kote duniani.

Msemaji wa kundi hilo, alisema kuwa walimuondoa waziri Haji Ghulam Bilour kwenye orodha ya watu wanaopanga kuwaua

Bwana Bilour aliahidi kutoa zawadi ya dola laki moja kwa yeyote atakayemuua mwenye kuitengeza filamu hiyo.

Serikali ya Pakistan imejitenga na matamshi ya waziri huyo lakini angali anashikila wadhifa wake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.