Makao makuu ya jeshi yashambuliwa Syria

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 12:33 GMT

Waasi nchini Syria wameshambulia na kuharibu vibaya makao makuu ya jeshi ambayo yalikuwa na ulinzi mkali mjini Damascus.

Televisheni ya taifa nchini humo iliripoti kuwa mabomu mawili yalilipuka, moja likilipukia ndani ya makao hayo.

Inaarifiwa kuwa waasi walifyatua risasi bado wakiwa ndani ya makao hayo ya jeshi.

Walioshuhudia tukio hilo walielezea kusikia ufyatulianaji risasi kwa masaa kadhaa ingawa duru za kijeshi zilisema kuwa hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Mwandishi wa gazeti la Sunday Times katika mji huo anasema milipuko miwili ilitangulia na kufuatiwa na mashambulio zaidi kutoka kwa vikosi vya waasi, ikiwemo makombora kabla ya makao hayo kuteketezwa moto.

Wanaharakati wanaopinga serikali, wameripoti kutokea vifo pande zote mbili.

Mwandishi habari wa kituo cha televisheni cha Iran Press Tv, aliuawa kwenye shambulio hilo. Duru za kidiplomasia zinasema kuwa maafisa wa usalama wamekuwa wakifanya msako wa nyumba hadi nyumba kuwakamata wale waliohusika na shambulizi hilo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.