Zahma kuhusu uchumi nchini Ugiriki

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 12:48 GMT


Ghasia zimezuka nje ya bunge la Ugiriki, kati ya polisi na waandamanaji ambao wameghadhabishwa na mpango wa serikali kupunguza matumizi ya pesa zake.

Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi, kujaribu kuwatawanya maelfu ya waandamanaji hao mjini Athens huku wakiwarushia polisi mawe na mabomu ya petroli.

Watu wengi wanashiriki mgomo wa siku moja ukiwa ndiyo wa kwanza tangu serikali mpya ya waziri mkuu mhafidhina Antonis Samaras, kuchukua uongozi mwezi Juni.

Mwandishi wa BBC mjini Athens anasema kuwa shughuli nchini kote zimekwama huku madaktari , walimu , wafanyakazi wa halmashauri ya kutoza kodi, wafanyakazi wa ferry na wale wa viwanja vya ndege, wakijiunga na mgomo huo kupinga mpango wa serikali kupunguza matumizi ya pesa za umma.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.