Aung San Suu Kyi asifiwa na Burma

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 16:47 GMT

Rais wa Burma, Thein Sein, amemsifu kiongozi wa upinzani nchini humo Aung San Suu Kyi kwa juhudi zake za kushinikiza demokrasia.

Akihutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa nchini Marekani, rais Thein Sein alimtambua kwa mara ya kwanza Aung San Suu Kyi kama mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na kumpongeza kwa tuzo alizopata akiwa nchini Marekani.

Suu Kyi alizuiliwa nyumbani kwake na serikali ya kijeshi kwa miaka kumi na tano. Mwanasiasa huyo aliwahi kuhudumu katika serikali hiyo.

Serikali ya sasa ya kiraia ya Burma, imeanza kufanya mageuzi tangu jeshi kukabidhi mamlaka kwa rais wa kiraia mwaka jana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.