Hofu ya miharadati nchini Peru

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 15:09 GMT

Ripoti ya Umoja wa mataifa imefichua kwamba ukuzaji wa mmea wa coca, unaotumika kutengeneza dawa ya kulevya ya Cocaine umeongezeka nchini Peru kwa mwaka wa sita mfululizo.

Ripoti hiyo kuhusu Dawa za kulevya na Uhalifu imedokeza kuwepo kwa ongezeko la asilimia mbili katika maeneo yanayokuza coca huko Peru mwaka uliopita.

Msemaji wa Umoja wa mataifa huko Lima ameonya kuwa wakulima wa mmea huo sasa wamepanua ukuzaji wa zamani kutoka maeneo ya Andes hadi kwenye mashamba yanayopakana na mpaka wa Brazil na Bolivia.

Aliongezea kuwa hadi wakati ambapo matumizi ya cocaine yatapungua hasa katika mataifa ya Bara Ulaya na Marekani, juhudi za kumaliza mmea wa coca huko Peru zitaambulia patupu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.