Takwimu za wakimbizi wa Syria zatisha

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 15:18 GMT

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR, limeonya kuwa idadi ya wakimbizi kutoka Syria wanaokimbilia usalama katika nchi jirani huenda ikatimu laki saba kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Shirika la UNHCR linasema Umoja wa Mataifa unaelekea kulemewa katika kulishughulikia tatizo hilo la wakimbizi na linahitaji Dola nusu bilioni kuwasaidia wakimbizi hao.

Afisaa mkuu wa umoja huo anayeshughulikia majanga ya kibinadamu Valerie Amos ameonya kuwa watu milioni 2.5 waliosalia ndani ya Syria wanahitaji msaada kufuatia mapigano yaliyokumba taifa hilo.

Takriban wakimbizi wapatao laki tatu wamevuka mipaka na kuingia katika nchi jirani za Jordan, Iraq, Iran Lebanon na Uturuki.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.