Waziri wa Pakistan hana majuto

Imebadilishwa: 28 Septemba, 2012 - Saa 09:29 GMT

Waziri wa reli nchini Pakistan Ghulam Ahmad Bilour aliyetangaza zawadi ya Dola laki moja kwa mtu yeyote atakayemuuwa mtengenezaji wa Filamu iliyowaghadhabisha Waislamu kote Ulimwenguni amesema hangetangaza zawadi hiyo iwapo mataifa ya Magharibi yangekuwa na sheria ya kukataza matukio kama hayo.

Wakati huo huo, mtu anayeshukiwa kutengeneza Filamu hiyo amesukumwa Jela kwa kukiuka masharti aliyowekewa kwenye kifungo chake cha nje na Mahakama ya Marekani.

Mshukiwa huyo mwenye asili ya Misri alizuiliwa baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka masharti hayo aliyowekewa tangu mwaka 2010.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.