Maandamano kupinga maduka India

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 12:40 GMT

Zaidi ya watu elfu moja wamefanya maandamano katika mji mkuu wa India , Delhi, wakipinga uamuzi wa serikali kuruhusu makampuni ya kigeni kuekeza katika biashara za masoko makubwa.

Maandamano hayo, yaliongozwa na waziri mkuu wa jimbo la Bengal,Magharibi Mamata Banerjee.

Chama chake cha kisiasa Trinamool Congress, hivi karibuni kiliwaondoa mawaziri wake kutoka kwa serikali ya taifa kuonyesha upinzani wake kuhusu sera hiyo.

Serikali imakubali kuruhusu maduka makubwa ya kifahari ya kigeni kufanya kazi nchini humo kwa ushirikiano na maduka ya nchini humo ingawa yatakuwa na umiliki mkubwa kuliko maduka ya nyumbani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.