Hofu ya wakongwe kuongezeka duniani

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 12:05 GMT

Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu wakongwe inaongezeka kuliko watu wenye umri mwingine wowote duniani na kwamba hali hii inahitaji kudhibitiwa hasa katika nchi zinazostawi.

Ripoti moja iliyotolewa na shirika la Umoja huo la kukadiria idadi ya watu duniani, inakariri kwamba, katika kipindi cha miaka kumi iyajo, idadi ya watu wataokuwa na zaidi ya umri wa miaka sitini itawadia bilioni moja.

Shirika la kuwahudumia wakongwe, la Help Age,ambalo limechangia ripoti hiyo, linatoa hamasa kwa nchi mbali mbali kuanzisha hazina bora zaidi za malipo ya uzeeni.

Ripoti hiyo inasema mikakati yenye mwelekeo mzuri kuhusu afya na ajira itahitajika ili kuimarisha hazina hizo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.