Mama kahaba kufunzwa dini

Imebadilishwa: 2 Oktoba, 2012 - Saa 15:31 GMT

Jaji mmoja Kaskazini Magharibi mwa Pakistan ameamuru mwanamke mmoja anayeshutumiwa kuendesha biashara ya danguro kujirekebisha kwa kuhudhuria masomo ya dini darasani katika msikiti kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.

Jaji Dost Mohammad Khan wa mahakama kuu ya Peshawar amefanya uhudhuriaji huo wa masomo ya dini kuwa kama sehemu ya masharti ya dhamana yanayotakiwa kutimizwa na mwanamke huyo.

Amemtaka Imam wa msikiti kuwasilisha ripoti ya maendeleo ya mwanamke huyo baada ya mwezi mmoja kukamilika.

Wachambuzi wanasema kuwa masharti ya mtu kubadilika kiroho yaliyotolewa na jaji huyo ni nadra sana kutolewa na pengine haikuwahi kutokea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.