Kero Iran kwa sarafu kushuka thamani

Imebadilishwa: 2 Oktoba, 2012 - Saa 14:55 GMT

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amelaumu kile alichokiita maadui wa nchi yake kama sababu ya kushuka kwa thamani ya sarafu yake, Rial.

Bwana Ahmadinejad amesema kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na nchi za Magharibi, vimesababisha kile alichokiita vita vya kiuchumi lakini hawataweza kukomesha mradi wa nuklia wa Iran.

Thamani ya Rial imeshuka, kwa asilimia kumi katika soko la hisa na sasa imepoteza thuluthi moja ya thamani yake katika kipindi cha zaidi ya wiki moja.

Benki kuu ya Iran, imesema kuwa dola elfu tano pekee ndiyo kiasi cha pesa ambazo msafiri anaweza kutoka au kuingia nazo nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.