'AL-Qaeeda ilianzisha moto msituni'

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 14:42 GMT

Afisaa mkuu mtendaji wa shirika la ujasusi la Urusi, FSB, Alexander Bortnikov, amesema kuwa moto uliozuka katika misitu na kusambaa hadi Kusini mwa bara Uropa na Balkans msimu wa joto, ulianzishwa na kundi la Al Qaeda.

Bwana Alexander aliyasema hayo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi mjini Moscow na kuonya kuwa watu walitumia mitandao inayomilikiwa na watu wenye siasa kali, kutuma habari kuhusu maeneo ya kuanzishia moto huo na ambavyo wataweza kuficha ushahidi.

Ingawa wanamazingira pamoja na makundi ya kutetea misitu, wanasema kuwa hakuna dalili kuwa moto huo ulianzishwa na makundi ya kigaidi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.