Waziri ajipata mashakani India

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 14:06 GMT

Waziri mmoja nchini India amejipata mashakani kwa kusema kuwa wanawake walioolewa huacha kuvutia na kupoteza urembo kila wanapozidi kuzeeka.

Waziri anayesimamia makaa ya mawe, Sriprakash Jaiswal, sasa anakabiliwa na kesi mahakamani kufuatia matamshi hayo aliyotoa katika mkutano wa kughani mashairi.

Akijitetea, Waziri huyo alisema alikuwa akifanya mzaha wakati alipokuwa akizungumzia kwa mlinganisho kuhusu mchezo wa Kriketi. Matamshi hayo yameibua tetesi kali kutoka kwa makundi ya kina mama.

Licha ya Jaiswal kuomba radhi, mwakilishi wa Shirika moja lisilo la serikali tayari amewasilisha kesi mahakamani akimlaumu Waziri huyo kwa kuwadharau wanawake.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.