Bwenyenye mashakani nchini Misri

Imebadilishwa: 4 Oktoba, 2012 - Saa 13:35 GMT

Mfanyabiashara mmoja shupavu nchini Misri, kutoka kwa uliokuwa utawala wa rais aliyeng'olewa mamlakani, Hosni Mubarak, ameamrishwa kulipa faini ya zaidi ya dola bilioni tatu na kutumikia kifungo cha miaka saba kwa kosa la ubini wa pesa.

Mfanyabiashara huyo, Ahmed Ezz, tayari anatumikia kifungo cha miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi mwaka jana.

Bwana Ezz alijipatia mabilioni ya pesa katika biashara zake za kutengeza chuma lakini ametuhumiwa kwa kutumia washirika wake wa kisiasa hasa na mwanawe Mubarak, Gamal kufanya ukiritimba kudhibiti soko la vyuma.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.