Waliuawa kwa kuaibisha familia India

Imebadilishwa: 5 Oktoba, 2012 - Saa 12:10 GMT

Mahakama moja nchini India imewahukumu kifo watu watano wa familia moja kwa mateso na mauji ya wapenzi wawili miaka miwili iliyopita.

Wapenzi hao waliuwawa na familia ya msichana huyo, ambayo ilipinga uhusiano wao kwa sababu mwanamume huyo alikuwa wa hadhi ya chini.

Wakereketwa wa haki za kibinadamu nchini humo wanasema mamia ya watu huuwawa kila mwaka kwa kupendana au kufunga ndoa kinyume na matarajio ya familia zao.

Mwaka uliopita, Mahakama ya Juu zaidi nchini India, ilisema mauaji kama hayo, yanapaswa kuadhibiwa kwa hukumu ya kifo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.