Kinyang'anyiro kikali nchini Venezuela

Imebadilishwa: 5 Oktoba, 2012 - Saa 10:42 GMT

Wagombea wawili wa urais nchini Venezuela wamehutubia umati mkubwa wa wafuasi wao katika siku ya mwisho ya kampeni kabla ya uchaguzi utakaofanyika Jumapili.

Rais Hugo Chavez ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka kumi na minne amewaambia maelfu ya wafuasi wake huko , Caracas kuwa anahitaji muhula wa tatu kuimarisha marekebisho ya kijamii na kutokomeza umaskini.

Naye mpinzani wake mkuu, Henrique Capriles, alikuwa na mikutano miwili katika miji ya magharibi.

Aliahidi kuimarisha uchumi na uongozi bora na kisha aliwahimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi Jumapili.

Aliwataka wapiga kura kumuunga mkono ili waweze kumshinda bwana Chavez kwenye uchaguzi huo siku ya Jumapili.

Wadadisi wanatabiri ushindani mkubwa kwenye uchaguzi huo dhidi ya Rais Chavez ukiwa ndio wa kwanza tangu aingine mamlakani mwaka wa 1999

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.