Mashambulizi Kusini mwa Israel

Imebadilishwa: 8 Oktoba, 2012 - Saa 12:38 GMT

Wanamgambo wa kipalestina katika ukanda wa Gaza wamerusha makombora na mizinga kusini mwa Israeli.

Makombora hayo yametua katika eneo lisilokaliwa na watu na hakuna taarifa za kuwepo kwa majeruhi .

Vugu vugu linalotawala Gaza la Hamas na kundi la kiislam la Jihad limesema lilirusha makombora hayo kulipiza kisasi mashambulio ya ndege za kijeshi yaliyofanywa na Israeli na kuwajeruhi wanamgambo wawili wa kipalestina, na raia wanane kwenye ukanda wa Gaza.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.