Wakamatwa kwa kuwaua wanafunzi Nigeria

Imebadilishwa: 8 Oktoba, 2012 - Saa 15:08 GMT

Polisi nchini Nigeria, wamewakamata zaidi ya watu kumi na wawili wanaohusishwa na mauaji ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Port Harcout.

Wanafunzi hao wanne waliuawa kwa kushambuliwa na genge la watu.

Inaarifiwa walivuliwa nguo na kutembezwa katika barabara za mji huo wakiwa uchi wakati wakichapwa na kisha baadaye kuteketezwa.

Kanda za video zikionyesha wanafunzi hao walivyokuwa wanatendewa , zilitolewa kupitia internet na kusababisha ghadhabu kote nchini humo.

Wanafunzi hao wanadaiwa kuiba simu za mkononi na komputa za laptop.

Mwanafunzi mwenzao mmoja, alisema kuwa wanafunzi hao waliuawa kimakosa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.