UN ilikosea kuhusu wanaokumbwa na njaa

Imebadilishwa: 9 Oktoba, 2012 - Saa 10:59 GMT

Umoja wa mataifa unasema kuwa ripoti yake ya mwaka 2008 ambayo ilisema kuwa watu bilioni moja duniani wanakumbwa na njaa haikuwa sawa.

Sasa umoja huo unasema kuwa ni watu milioni 870 ambao wanaishi bila chakula.

Katika ripoti yake ya kila mwaka , shirika la umoja huo la chakula na kilimo , limesema limebadili ambavyo kawaida hujumlisha takwimu zake, na sasa linatumia mbinu ambazo ni za uhakika.

Kwa mujibu wa shirika hilo, idadi ya watu amabo wanakumbwa na njaa , imekuwa ikipunguka wala sio kuongezeka angalau katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita. Hata hivyo tangu msukosuko wa uchumi kuanza kutokea duniani, hali imedumaa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.