Njama ya wafuasi wa Laurent Gbagbo

Imebadilishwa: 9 Oktoba, 2012 - Saa 16:00 GMT

Ripoti ya Umoja wa mataifa inasema wafuasi wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, wamekuwa wakijaribu kupata usaidizi kutoka kundi la wapiganaji wa Kiislamu kutoka Mali kwa ajili ya kampeini ya kuzusha ghasia nchini Ivory Coast.

Ripoti hiyo pia inawashutumu wafuasi wa Bwana Gbagbo kwa kujaribu kuchukua wanajeshi wa vikosi vya Mali kuwasaidia kunyakua madaraka kutoka kwa Rais wa sasa Bwana Alassane Ouattara.

Bwana Gbagbo anasubiri kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai.

Wafuasi wa Bwana Gbabo wameielezea ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa ni uongo wa kimakusudi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.