Papa ahubiri kwa Kiarabu

Imebadilishwa: 10 Oktoba, 2012 - Saa 15:33 GMT

Papa Benedict wa kumi na sita, ametoa baraka zake kwa lugha ya kiarabu katika hotuba yake ya kila wiki kwa dunia nzima.

Hotuba hiyo hupeperushwa moja kwa moja kupitia televisheini.

Papa alisema kuwa anawaombea watu wote wanaotumia lugha ya Kiarabu.

Kabla ya maombi yake, padri mmoja pia alisoma hotuba ya wiki kwa mara ya kwanza katika lugha ya Kiarabu.

Maafisa katika makao makuu Vatican walisema kuwa hatua hiyo huenda itawafarijji wakristo Mashariki ya kati , wengi wao ambao wamekuwa wakiondoka kutoka eneo hilo wakisema kuwa wanahofia usalama wao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.