Watetea haki za wanawake Afghanistan

Imebadilishwa: 10 Oktoba, 2012 - Saa 14:00 GMT

Wanaharakati zaidi ya 80 wanaotetea haki za wanawake nchini Afganistan wanafanya mkutano na viongozi wa kidini nchini humo kama njia moja ya kuwashinikiza kuunga mkono haki za wanawake nchini humo.

Wanaharakati hao wakiwemo wawakilishi kutoka serikalini wanataka hatua zaidi zichukuliwe kukomesha dhuluma dhidi ya wanawake haki ya kupata elimu na ajira sambamba na haki zao za kidini .

Hivi karibuni shirika huru la kutetea haki za kibinadamu nchini Afganistan liliripoti ongezeko la dhuluma dhidi ya wanawake ikiwemo ubakaji na mauaji.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.